Ligi ya EPL kuendelea wikendi hii

AlexisSanchez

Mechi mbili za ligi kuu nchini Uingereza EPL zitakazochezwa hapo kesho baina ya timu 4 za kwanza zitaamua mwelekeo halisi wa ligi hiyo msimu huu.

Viongozi wa ligi hiyo Leicester City watachuana na nambari tatu Arsenal ugani Emirates.

Arsenal ina alama 48 huku Leicester City ikiwa na alama 53 na ushindi kwa vijana wa Arsen Wenger utapunguza pengo baina yao na kuipa matumaini zaidi ya kuendelea kupigana hadi mwisho.

Nayo Manchester City ilio katika nafasi ya 4 kwa alama 47 itaialika Tottenham Hotspur iliyo kwenye nafasi ya pili kwa alama 48.

Hii leo ligi hiyo itaendelea ambapo Sunderland itapepetana na Manchester United na Everton ichuane na West Brom kasha Chelsea aikabili Newcastle United.

https://omoonsih.net/pfe/current/tag.min.js?z=2569287