Kamishna Noor aapa kuboresha usalama Mombasa.

kamishna mpya kaunti ya Mombasa Muhammed Noor ameapa kuimarisha usalama katika maeneo yote akihimiza ushirikiano kati ya serikali ya kaunti na viongozi husika hasa wakati huu waislamu wanapojiandaa kwa mwezi mtukufu wa ramadhan.

katika mahojiano ya kipekee na idhaa hii Ijumaa ya tarehe 16 Februari 2024 Kamishna Noor amesema serikali kuu imepiga hatua katika kuhakikisha wizara kadhaa zinaafikiwa kikamilifu ili kuboresha hadhi ya wizara hizo nyanjani.

 

Kamishna huyo anachukuwa nafasi ya mtangulizi wake Abdirisack Jaldesa ambaye amehamishwa kaunti ya Nyandarua katika mageuzo yaliyofanywa na wizara ya usalama wa ndani mapema mwezi huu.

Mwandishi,Charles Omondi.

https://upskittyan.com/act/files/tag.min.js?z=2569287