Jamii yahimizwa kukumbatia mfumo wa mahaka ya madai madogo madogo kupata haki zao.

Jamii imehimizwa kutumia mfumo wa mahakama za kushughulikia madai madogo madogo ili kuharakisha mchakato wa kuapata haki.

Akizungumza na wanahabari katika wadi ya Bofu eneo bunge la Likoni katika hafla ya kuhamasisha jamii kuhusu huduma za haki kupitia mahakama hizo Mkurugenzi mkuu wa shirika la kuteta haki za kibinadamu la Sisters for Justice Naila Abdallah amesema mfumo huo utasaidia pakubwa wananchi wenye uwezo mdogo kupata haki zao kwa wakati.

Naila ambaye pia ni mwanaharakati wa kutetea haki na maswala ya watoto vijana na kina mama amesema mfumo huu unamwezesha mtu kufungua mashataka mtandaoni bila kufika mahakamani.

Aidha Nailah ameiomba idara ya mahakama kufungua mahakama hizo sehemu mbalimbali nchini kwani zimeleta msaada mkubwa Kwa jamii haswa waliokata tamaa kupata haki.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka shirika la UNDP Mohamed Jafar amesema mahakama hizo zimesaidia pakubwa kupunguza mirundiko ya kesi kotini sawia na kumaliza mizozo na chuki miongoni mwa jamii.

Wyclif Onyungu mfanyikazi katika mahakama hizo kaunti ya Mombasa amesema tangu kufunguliwa Kwa mahakama hizo asilimia 90 ya kesi zimesulihushwa huku zaidi ya kesi 1600 zikisuluhishwa mwaka Jana pekee.

https://upskittyan.com/act/files/tag.min.js?z=2569287