VANGA UNITED -MABINGWA KHAIRAT MFUNGO CUP

Vanga United ndio mabingwa wa michuano ya KHAIRAT MFUNGO CUP baada ya kuwachabanga Kiwegu united goli moja Kwa nunge.
Goli hilo lilitiwa wavuni kunako dakika ya 30 na mshambuliaji machachari wa Vanga United Majam Abdallah almaarufu Etoo ambae pia aliebuka kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo Kwa kufunga jumla ya magoli mawili .
Michuano hiyo ilivutia timu nne kutoka vijiji vinne vya Vanga,Kiwegu,Jasini na Jego ambapo Kila Kijiji kilitoa timu moja.
Ligi hiyo ambayo ilianza katika hatua za muondoano iliwakutanisha timu ya Vanga na Jasini ambapo Vanga United waliizaba Jasini FC magoli matano Kwa yai.

Mechi ya pili ilikuwa kati ya Kiwegu FC na Jego FC ambapo KIWEGU waliebuka na ushindi wa goli moja Kwa nunge na kujikatia tiketi ya fainali huku
Mshindi watatu wa michuano hiyo akiibuka Jasini baada ya timu ya Jego FC kukosa kufika uwanjani.
Mgeni wa heshima kwenye fainali ya ligi hiyo ,ambaye pia ni mwanasiasa aliyewahi kugombea kiti cha Useneta katika kaunti ya Kwale,Salim Ali Mwadumbo, ameahidi kutambua na kukuza talanta miongoni mwa vijana kwenye kaunti hiyo huku akisisitiza haja ya ushirikiano kati ya wadau wa maswala ya soka na viongozi Ili kufanikisha hilo.

Mwadumbo Aidha amesema kuwa atashirikiana na viongozi wa timu mbali mbali Ili kuwawezesha kupata mahitaji au vifaa hitajika katika timu zao huku akiahidi kuandaa ligi kubwa zaidi ambayo itavutia timu zaidi katika wadi ya Vanga ambapo mshindi ataondoka na zawadi nono.
Katika ligi ya KHAIRAT MFUNGO CUP awamu ya kwanza,mshindi Vanga United alizawadiwa kitita cha shilingi elfu 20 pesa taslimu na jezi, huku mshindi wa pili KIWEGU FC akipata shilingi elfu 15 na jezi, Timu iliyofanikiwa kuibuka ya tatu katika michuano hiyo Jasini Fc akizawadiwa shilingi elfu 10 na jezi huku timu iliyoibuka ya nne jego FC wakipata 5k na jazi.

Kadhalika Mfungaji bora Majam Abdallah alipata zawadi ya mpira huku refa bora Majambo Amsha akipata zawadi sawia na hiyo.
Kwa upande wao waandalizi wa ligi hyo wakiongozwa na Maftaa Juma wamezishukuru timu hizo Kwa kuonyesha ushirikiano na kiwango kikubwa Cha nidhamu wakati wa michezo yao huku wakiahidi kuandaa ligi zaidi za kutambua na kukuza talanta.
Aidha waandalizi wamewaomba wadhamini zaidi pamoja na washikadau na serikali ya kaunti kudhamini michuano kama hiyo Ili kuwashughulisha vijana na kuwaepusha kujiingiza katika anasa na utumizi wa dawa za kulevya,sawia na kushirikiana na makundi ya vijana kuandaa ligi kama hizo mashinani.
