Radio Salaam ni stesheni ya kitaifa nchini Kenya iliyoanzishwa rasmi mnamo tarehe 16 Novemba mwaka wa 2006. Radio Salaam inapeperusha matangazo yake kutoka mji wa Mombasa kwa Lugha ya Kiswahili kupitia mfumo wa mazungumzo na habari kila baada ya saa.
Radio Salaam inajivunia kuwa na Vipindi vya kusisimua vyenye ufuasi mkubwa Kenya nzima kama vile, Kauli Yako, Farashani, Uteo, Dini ya Mitume, MV Salaam, Jukwaa Wazi, Ukwasi wa Kiswahili na Kongamano.
Vipindi hivi vinalenga kuboresha jamii kupitia mada mbalimbali, hasa kuhusiana na; siasa, Elimu, uchumi, matukio ulimwenguni, michezo, masuala ya Wanawake, Vijana, Walemavu na Watoto.
Radio Salaam inafurahia kuwa na watangazaji wanaotajika nchini Kenya kwa kubobea katika fani ya uandishi wa habari. Hili limedhihirishwa na ubingwa wa wanahabari wetu katika tuzo za kitaifa za kuwatunuku wanahabari bora kila mwaka. Miongoni mwa mashindano hayo yakiwemo, EJEA, AJEA, TUVUKE, na INTERNEWS.
Wafikie wateja wako Kupitia Radio Salaam.
Tuna uhusiano wa kudumu na wasikilizaji wetu wapatao milioni 10 wakiwemo watu kutoka matabaka mbali mbali ya kijamii, kiuchumi na kidini wanaotegea.
Kuwa stesheni la kipekee katika maeneo ya pwani lenye gari lililo na mitambo ya kisasa ya kupeperusha matangazo kutoka mahali popote inawapa fursa wateja wetu wenye hafla wanazotaka ziangaziwe zinapoendelea.
Tuma ujumbe kupitia dawati letu la biashara kupitia barua pepe kwa: sales@radiosalaamfm.com