Mashirika yaungana kuhimiza Wakaazi wa Kisauni kutunza mazingira ya bahari.
Wakaazi katika eneo bunge la kisauni kaunti ya Mombasa wamehimizwa kutunza fuo za bahari kwa kuhakikisha wanadumisha usafi pamoja na kupanda miti aina ya mikoko ili kuimarisha mazingira ya bahari.
Akiongea na waandishi wa habari baada ya zoezi la kusafisha fuo ya bahari ya Manyani na kupanda miti aina ya mikoko iliyoongozwa na shirika la jamii la akili kadhaa kwa ushirikiano na mashirika mbalimbali Mwenyekiti wa mradi wa Lapset Ali Mbogo amesema zoezi hilo linaumuhimu mkubwa haswa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Mbogo ambaye aliwahi kuhudumu kama mbunge wa kisauni amepongeza juhudi za shirika hilo kwa kuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa zoezi hilo.
Aidha Mbogo ameweka wazi kuwa jitihada zake za kusaidia wakaazi wa kisauni si kwa ajili ya kisiasa bali ni kuwawezesha kujikimu kimaisha.
Kwa upande wake mwenyekiti wa shirika hilo Juma Mashuhuri amesema wameweka mikakati kabambe ya kuwahamasisha na kuwafunza jamii kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira ya bahari kwa manufaa ya viumbe vya baharini nan chi kazi.
Mashuhuri akiwataka wakaazi kutupilia mbali tofauti zao kisiasa na kushirikiana katika shughuli za maendeleo kwa manufaa yao na vizazi vya baadae.
Shughuli hiyo iliyoanza leo rasmi na kuongozwa na shirika la Akili Kadhaa itachukua muda wa miezi sita NA imefadhiliwa na mashirika mbalimbali ikiwemo mamlaka ya bahari nchini KMA na kemfri.
Zaidi ya miche 500 ya mikoko imepandwa katika awamu ya kwanza ya mradi huo.