Watanzania Wapiga Kura Huku Magufuli akijipa Tumaini ya Tano Tena

Watanzania hii leo wanashiriki upigaji kura  katika uchaguzi mkuu ambapo Rais John Magufuli anatumai kushinda muhula mwingine wa miaka miaka mitano kuliongoza taifa la Tanzania lilioko kanda ya Afrika Mashariki.

Katika Mchakato huo Wapinzani wakuu wa Magufuli ni mgombea mtelule wa chama cha Cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA Tundu Lissu pamoja  na Bernard Membe wa chama cha ACT Wazalendo.

Ni uchaguzi mkuu wa sita tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992. Hapo jana wakaazi wa visiwani Zanzibar walianza kupiga kura lakini awamu ya jana ilikuwa inahusisha makundi maalum.

Katika muda mfupi ujao vituo vya kupigia kura vitafunguliwa ambapo kwa mujibu wa maafisa wa uchaguzi, zoezi hilo litaendelea hadi saa kumi na mbili jioni kabla ya kuanza shughuli ya kuhesabu kura hizo huku Zaidi ya watu milioni 30 wamesajiliwa kupiga kura kati ya raia milioni 58. Watamchagua rais kutoka kwa wagombea 15 na kuwachagua wawakilishi wao katika bunge lenye viti 264.

Hata hivyo Zanzibar ina historia ya mazingira tete ya uchaguzi yanayokumbwa na machafuko na makosa na upinzani kwa mara nyingine umekituhumu chama tawala cha CCM kwa kutaka kuiba kura. Kisiwa hicho kilipiga kura ya mapema jana kwa vikosi vya usalama na makundi mengine maalum ambapo ghasia zilizuka na kusababisha vifo vya watu 10 na wengine kujeruhiwa.