Shirika la Usawa Agenda lazindua ripoti ya Elimu Ukanda wa Pwani.

Shirika lisilokuwa la kiserikali la Usawa Agenda kwa ushirikiano na mashirika mbalimbali ya kijamii ukanda wa pwani yamezindua ripoti maalum inayofahamika kama Foundation Literacy and Numeracy Assessment FLANA yenye tathmini ya viwango vya elimu eneo la pwani .
Hii baada ya utafiti uliofanywa katika kaunti zote 47 nchini mwaka uliopita ili kutathmini viwango vya kusoma ,kuandika na kuhesabu miongoni mwa watoto wenye umri wa miaka kati ya 6 -16 ili kuchochea sera zenye ushahidi ambazo zingeweza kusababisha ujifunzaji sawa kwa watoto wote .
Mratibu wa shirika la Usawa Agenda kaunti ya Kwale ambaye pia ni mwanachama wa shirika la kijamii la Kwale Youth and Governance Consortium KYGC Amani Lugogo amesema kuwa utafiti huo ulijumuisha vijiji 230 ,nyumba 6,348 , watoto 3,016 na shule 226 ukanda wa pwani .

https://couphaithuph.net/act/files/tag.min.js?z=2569287