Matiangi azindua kituo cha kukabili ugaidi Mombasa
Serikali ya Kenya Kwa Ushirikiano na Ile uingereza imezindua jengo la makao makuu ya kitengo cha kukabiliana na Ugaidi katika kanda ya pwani. Uzinduzi wa jengo hilo lililogharimu jumla ya shilingi milioni themanini na moja umetajwa kama hatua muhimu itakayoimarisha vita dhidi ya Ugaidi Nchini .
Akizungumza Mjini Mombasa wakati wa Uzinduzi rasmi wa jengo hilo, Waziri wa usalama wa ndani Dakta Fred Matiang’i amesema kuwa taifa la Kenya limekuwa likiimarisha mikakati yake kukabiliana na tatizo la ugaidi , Huku akiahidi kuwa idara ya usalama nchini itazingatia Haki za binaadamu wakati wa kuwazuia washukiwa wa Ugaidi.
Hata hivyo Matiang’i amepongeza hatua hiyo huku akisema kuwa Serikali ya Kenya itaendeleza mijengo ya aina hiyo katika maeneo mengine Nchini ili kukabiliana kikamilifu na ugaidi.
Kwa upande wake Balozi wa Uingereza Hapa Nchini Jane Marriot amesema uingereza itaendelea kuunga mkono Kenya katika vita vyake dhidi ya ugaidi kwa kutoa mafunzo ya hali ya juu kwa maafisa wa polisi wanaokabiliana na ugaidi ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao ipasavyo.