Rais mteule John Pombe Magufuli aapisha kwa muhula wa pili

Picha kwa hisani

 

Rais mteule wa Tanzania John Pombe Magufuli ameapishwa rasmi kama rais wa nchii hiyo kwa muhula wa pili kwa mujibu wa katiba .

Maguli alimbaga mpinzani wake wa karibu Tundu Lissu kwa ushindi mnono .

Kwenye hotuba yake magufuli amewashukuru watanzania waliompigia kura  na kuonyesha utulivu mkubwa na kusema kuwa wamekua kidemokrasia akiongezea ya kwamba ushindi huo ni wa watanzania wote.

Vilevile amesisitiza kuhusu maendeleo akisema kuwa uchaguzi umeisha na ni sharti swala la maendeleo iwe msingi.

“uchaguzi sasa umekwisha . Jukumu kubwa ni kuendeleza jitihada la kulijenga na kuleta maendeleo kwa taifa taifa letu,” Magufuli ananukuliwa.

Swala la ahadi pia limegusiwa kwenye hotuba hiyo huku Rais John Maguli akiwahakikishia watanzania kuwa atatimiza ahadi zote alizozitoa zikiwemo kujenga Tanzania itakayojitegemea , kulinda na kudumisha amani , kukamilisha miradi na kuimarisha usimamizi wa raslimali.

Aidha , ameahidi kukuza uchumi na kushughulikia changamoto za kiuchumi na ukosefu wa ajira.

Ameapa kupambana na ufisadi nchini humo kwa ushirikiano na watanzania.

Rais huyo ameshukuru chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kumpigia debe na kupongeza wabunge waliochaguliwa kupitia chama hicho.

Sherehe hiyo imeshunduriwa na maelfu ya watanzania na viongozi mbalimali wakiwemo  marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi, Jakaya Kikwete , rais wa Uganda Yoweri Museveni na rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa.

 

 

 

https://vaugroar.com/act/files/tag.min.js?z=2569287