Supkem yakashifu Kuteketezwa kwa Qur’an takatifu nchini Sweden
Ofisi ya Mwenyekiti wa kitaifa wa baraza kuu la Waislamu hapa nchini Supkem imeungana na Serikali na taasisi nyengine kote Ulimwenguni kukashifu kitendo cha Kuteketezwa kwa Kitabu kitakatifu cha Qur’an,nje ya ubolozi wa Uturuki nchini Sweden, kilichotekelezwa na Mwanaharakati wa kisweden anayepinga dini uislam Rasmus Paludan,chini ya uangalizi wa maafisa wa Polisi.
Katika taarifa yake kwa Vyombo vya Habari Baraza la Supkem limesema kuwa japo linaufahamu wa uhuru wa kijieleza na kuwa na imani tofauti lakini kitendo hicho Cha Kutekeketeza Kitabu Qur’an takatifu nje ya ubolozi wa taifa hilo ambalo idadi yake kubwa jamii ya waislamu, Kimedhihirisha itikadi potovu na chuki dhidi watu wa jamii hiyo Ulimwenguni.
Wakati huo huo Baraza la Supkem Kupitia mwenyekiti wake wa Kitaifa Al hajj Hassa Ole Naado limewataka raia wa Sweden pamoja Serikali ya nchini humo kupinga kitendo hicho cha chuki kilichotekelezwa na Paludan kwa kuchukua hatua dhidi yake , likiyarai mataifa mengine kote ulimwenguni kutokubali Vitendo vya itikadi kutekelezwa katika ardhi zao.
Baraza Supkem hatahivyo ulimewatolea wito waislamu kote ulimwenguni waliochukizwa na kitendo hicho kujidhibiti na kuepuka vitendo vyovyote vya ghasia vya kulipiza kisasi vinavyomlenga mwanaharakati huyo au taasisi zinazojihusisha naye.