Waandishi katika kaunti ya Mombasa wahimizwa kuripoti habari za upekuzi.
Waandishi katika kaunti ya Mombasa wamehimizwa kuboresha uandishi wao kwa kuripoti habari za upekuzi ili kueleza wananchi ni yapi yanayofanyika katika sekta mbalimbali za kiserikali.
Akiongea na mwanahabari wetu mratibu WA Kanda ya Pwani katika Baraza la vyombo vya habari nchini Maureen Mudi amesema licha ya kuwa na changamoto zake inaleta taswira yakuonyesha ni jinsi gani unatambua utendakazi wako Kwa kuwaeleza jamii Yale yote yanayofanyika bila wao kujua.
Aidha Maureen amesema waandishi wanafaa kufanya utafiti katika vyanzo mbalimbali vya serikali kabla ya kuripoti au kuchapisha taarifa zao ili kuzipa uzito taarifa zao.
Haya yanajiri huku zaidi ya wanahabari 20 kaunti ya Mombasa wakiendelea na mafunzo ya siku nne kuhusu kuandika taarifa za upelelezi zinazohusu sekta na masuala ya afya.
Mafunzo hayo yanadhaminiwa na Muungano wa Wanahabari wa Kike nchini Kenya (AMWIK) kwa ushirikiano na shirika la Marekani Misaada na Maendeleo (USAID).