Naibu Chifu Asalia Rumande kwa tuhuma za Ubakaji
Naibu mmoja wa chifu kutoka kaunti ya Machakos ambaye alikamatwa mwezi Juni kwa tuhuma ya umbaka wa mwanafunzi wa darasa la nane mwenye umri wa miaka 16 atasalia rumande hadi pale uchunguzi utakapomalizika.
Haya ni kulingana na hakimu wa Machakos Charles Odiek ambaye ameagiza mshukiwa huyo kwa jina Daniel Wambua kusalia kwenye rumande hadi mwezi Agosti tarehe 6 wakati mahakama itakapoamua kuhusu ombi lake la dhamana.