Seneta Sakaja Atozwa faini ya Kshs. 15 Elfu Au kifungo miezi 3

photo courtesy; google

Seneta wa Nairobi Johnson Sakaja ametozwa faini ya shilingi elfu 15 au kifungo cha miezi mitatu gerezani baada ya kuwasilishwa mahakamani hii leo kufuatia kesi inayomkabili ya kukiuka sheria ya kafyu.

Kesi hiyo iliyosikilizwa na hakimu mkuu Roselyn Oganyo katika uwanja wa michezo wa kasarani jijini Nairobi, Sakaja ametakiwa kuweka wazi hatua yake ya kujihuzulu kutoka kwa kamati ya bunge iliyobuniwa kushughulikia janga la korona kwa maandishi.

Amesema hatua hiyo ndio itakuwa thibitisho kamili kwa mahakama sawia na wakenya kwa ujumla kuhusiana na hatua yake aliyochukua ya kujihuzulu kutoka kwa kamati hiyo.

Mahakama imesema kuwa sakaja alistahili kuonyesha mfano bora kwa wakazi wa Nairobi na taifa kwa ujumla ikizingatiwa kwamba visa vya maambukizi vinazidi kuongezeka kila siku hasa katika kaunti ya Nairobi.

Ikumbukwe kuwa Sakaja alishikwa siku ya jumamosi saa saba usiku katika mkahawa mmoja jijini Nairobi akibugia mvinyo akiwa na wenzake.

mwandishi; Geoffrey Chiro.