Uchaguzi wa Ugavana Mombasa kuahirishwa endapo Mahakama itaamuru hivyo
Huenda uchaguzi wa kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa ukahairishwa endapo mahakama itaamuru hivyo.
Mwenyekiti wa Tume huru ya uchaguzi na mipaka Wafula chebukati amesema kuwa hatua hiyo itachukuliwa kwa maeneo ambayo yanakumbwa na kesi mbali mbali ikiwemo ile ya Mike Mbuvi Sonko ambayo iko kwa mahakama ya Afrika mashariki ya Haki.
Kauli ya Chebukati inajiri baada ya Sonko kupeleka kesi yake kwa mahakama ya Afrika mashariki baada ya cheti chake kutupiliwa mbali na Tume hiyo kufuatia uamuzi wa Mahakama ya upeo.
Hata hivyo Chebukati ameweka wazi kwamba agizo la mahakama ya afirika mashariki kuhusu ombi la Sonko kuwania ugavana Mombasa katika uchaguzi ujao halijapokelewa na Tume ya IEBC.