Sonko aidhinishwa na IEBC kuwania ugavana Mombasa
Ni rasmi sasa aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko atawania kiti cha ugavana Mombasa baada Tume huru ya Uchaguzi na mipaka IEBC kumuidhinisha kuwania kiti hicho
Akizungumza wakati wakukabidhiwa cheti na tume hiyo sonko ameeleza kuwa yupo tayari katika kinyang’anyiro hicho licha ya mda mchache uliosalia taifa kuingia katika uchaguzi mkuu huku akiipongeza mahakama Kwa kusimama na haki huku akiwasuta wanaoikashifu nakuitaja mahakama kutoegemea upande wowote.
Aidha ameahidi kuimarisha uchumi wa kaunti hiyo pamoja nakuunda serikali itakayounganisha makabila yote sawia na kuimarisha miundo msingi pindi tu atakapochaguliwa kuhudumu kama gavana wa Mombasa nakuwataka wafuasi wake kudumisha amani kipindi cha kampeni.
Kwa upande wake Mgombea mwenza wa Sonko Ali Menza Mbogo ameeleza kuwa wao kama wagombea wako tayari kuminyana na wapinzani wao kwa mda ulio salia nakuahakikisha kutembeza sera zao hadi mashinani.