Muhuri mahakamani
Shirika la kutetea haki za kibinadamu la MUHURI limetishia kuelekea mahakamani kuishtaki serikali kuu kufuatia kufungiwa kwa wakazi wa mtaa wa old Town mjini Mombasa kutotoka wala kuingia eneo hilo baada ya maambukizi ya virusi vya korona kuzidi kwenye mtaa huo.
Kulingana na Mkurugenzi wa shirika hilo Khelef khalifa, wakaazi wa mtaa huo walipata madhara makubwa ya kiuchumi kipindi hicho cha kufungiwa kwa wenyeji wa mtaa huo.
Amesema kwamba serikali haikuweka wazi sababu za kufunga mtaa huoakisema kwamba ripoti waliyopata kutoka kwa serikali haikuwa ya manufaa yoyote bali yalikuwa ya kugandamiza mwananchi wa kawaida.