Kwa mara nyengine Sonko apata pigo baada ya mahakama ya upeo kutupilia mbali rufaa.
Kwa mara nyengine ni pigo kwa aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko baada ya Mahakama upeo Nchini kutupitilia mbali rufaa kuwa aliondolewa mamlakani kama Gavana Wa Kaunti ya Nairobi kinyume na Sheria.
Katika Uamuzi Mahakama hiyo kupitia Kwa jopo la majaji Saba liloongozwa na jaji mkuu Martha Koome limeafikiana na uamuzi wa awali wa mahakama za chini kuwa Bunge la seneti lilifuata Sheria kumbandua Sonko kutoka Kwa wadhafa wale wa Ugavan.
Uamuzi wa Mahakama hiyo ya upeo unaamanisha kuwa Sonko amefungiwa nje ya kinyang’anyiro cha Ugavana katika Kaunti ya Mombasa baada ya kumaliza rufaa zake zote za kupinga kunga’tuliwa mamlakani
Ikumbukwe kuwa uamuzi huo wa mahakama ya upeo unajiri siku moja Tu baaa ya Tume ya IEBC kumuidhinisha Sonko kuwania Ugavana katika Kaunti ya Mombasa