Maraga afungua rasmi kongamano la majaji Mombasa

PHOTO: Courtesy

By Mohamed Mutakina

Jaji mkuu David Maraga amefungua rasmi kongamano la kila mwaka la majaji na ambalo litaendela kwa siku nne hapa Mombasa.

Katika Hotuba yake ya ufunguzim,  Maraga amegusia maswala mbali mbali ambayo yanalenga kujadiliwa wakati wa vikao hivyo, akitilia mkazo uhuru wa idara ya mahakama, mrundiko wa kesi mahakamani pamoja na maadili ambayo anasema yatachangia kwa  wananchi kuwa na imani na idara hiyo.

Aidha, Maraga amedokeza kwamba kufikia mwezi juni mwaka huu idadi ya kesi zilizozidi miaka mitano zimepungua kwa kiasi kikubwa.

Zaidi ya majaji 150 wanahudhuria kongamano hilo ambalo mada kuu ni kusawazisha uhuru na uwajibikaji wa kisheria.

 

 

 

 

https://vaugroar.com/act/files/tag.min.js?z=2569287