Kesi ya magavana dhidi ya Serikali kuu yang’oa nanga leo
Mahakama ya juu hii leo imeanza kikao cha kusikiliza kesi iliyowaslishwa na magavana kulishtaki bunge la kitaifa kwa kuzitengea serikali za kaunti shilling billoini mia 316 badala ya shilling billioni mia 335
Jaji mkuu David Maraga anaongoza jopo la majaji wanaosikiliza kesi huku kwa sasa mawakili wa pande zote mbili wakiwa wanatoa hoja zao
Ijumaa wiki iliyopita jaji mkuu David Maraga aliwaagiza mawakili wote wanaowakilisha magavana kuhakikisha stakabadhi zote zinawasilishwa mahakamani kufikia jumatatu wiki hii kabla kesi hiyo kutajwa na kusikilizwa
Magavana hao aidha wanataka mahakama hiyo kutoa mwelekeo kuhusu mapendekezo ya mamlaka ya ugavi wa mapato ambayo wanadai unapuuzwa na bunge la kitaifa