Waititu azuiliwa kuingia katika afisi za kaunti yake
Gavana wa kaunti ya Kiambu Ferdinand Waititu maarufu kama Baba Yao amezuiwa kuingia katika afisi zake. Hakimu Larence Mugambi amesema kuwa Waititu na washukiwa wengine ambao ni wafanyikazi wa kaunti hiyo hawataruhusiwa kuingia afisini hadi kesi hiyo itakapomalizika ili kutotatiza ushahidi.
Aidha Waititu ameachiliwa huru kwa dhamana ya shilingi milioni 15 huku Mkewe Waititu Susan Wangari naye ameachiliwa huru kwa dhamana ya shilingi milioni 4.
Washukiwa wengine katika sakata hii ya ufujaji wa shilingi milioni 588 pesa za kaunti wemeachiliwa huru kwa dhamana ya shilingi milioni 15 na milioni 4.
Kesi hiyo sasa itatajwa tarehe 26 Agosti mwaka huu