Winnie Mandela akosa kurithi nyumba ya Mandela

Aliyekuwa mkewe Nelson Mandela amepoteza harakati zake za kutaka kurithi makao yalio mashambani ya rais huyo wa zamani wa taifa la Afrika Kusini.

Mahakama kuu ya Mthatha ilipuuzilia mbali ombi la Winnie Madikizela Mandela na kumtaka alipe gharama zote za kesi hiyo.

Winnie alidai kuwa nyumba hiyo ambapo Mandela alihudumu muda wake mrefu hadi kifo chake mwaka 2013,ni mali yake kulingana na sheria za kitamaduni.