Boko Haram 800 wajisalimisha

Wapiganaji 800 wa kundi la wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram wamejisalimisha kwa jeshi la Nigeria.

Hatua hiyo inafuatia mpango wa Operation Safe Corridor unaolenga kuwapokea wapiganaji wa kundi hilo la kigaidi ambalo limesababisha vifo vya maelfu ya raia wa nchini Nigeria.

Katika mpango huo wapiganaji wanaojisalimisha wanachukuliwa na kufunzwa njia mbadala ya kujitafutia riziki.

Msemaji wa jeshi amesema kuwa wanania ya kuwasamehe wapiganaji wa Boko Haram watakaojisalimisha.

Kwa sasa wamewekwa kwenye makazi maalum ambapo wanaendelea kupata mafunzo.

Baadaye watafunzwa mbinu mpya za kujitafutia riziki kabla ya kupewa mtaji wa kuanza upya maisha yao.

Hata hivyo kuna hofu iwapo jamii itakuwa tayari kuwapokea wapiganaji waliotekeleza maasi dhidi yao.