Waziri wa zamani wa Rwanda afariki

Waziri wa zamani wa Rwanda Jacques Bihozagara amefariki katika gereza moja nchini Burundi miezi minne baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kufanya ujasusi.
Rwanda imesema marehemu Jacques alikuwa ameshikiliwa kinyume cha sheria na Balozi wa nchi hiyo nchini Ubelgiji.
Wafungwa katika gereza alipokuwa ameshikiliwa wanasema alionekana akiwa katika hali nzuri na kwamba alifariki dakika chache baada ya kuchuKUliwa katika gereza kupelekwa hosptali baada ya kuugua.
Umoja wa Mataifa umekuwa ukiishutumu Rwanda kwa kujaribu kuipindua serikali ya Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, madai ambayo Rwanda imekuwa ikiyakanusha.