Mehbooba Mufti aapishwa kuwa mwanamke wa kwanza kuchukua madaraka ya Waziri jimbo la Kashmir India

 

Mehbooba Mufti ameapishwa kuwa mwanamke wa kwanza kuchukua madaraka ya Waziri kiongozi wa jimbo la Kashmir nchini India.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 56 ni mtoto wa waziri kiongozi wa zamani, Mufti Mohammed Sayeed aliyefariki mwezi Januari.

Kifo cha Babake kilisababisha hali ya mvutano kati ya Mehbooba na Chama tawala nchini India,BJP kuhusu mustakabali wa serikali ya pamoja.