Ebola sio janga tena yasema WHO

Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa Ebola sio janga tena la kiafya na kwa sasa hatari ya kusambaa kwa virusi vya ugonjwa huo ni kidogo.
Visa kidogo bado vinaripotiwa nchini Guinea, huku Sierra Leone na Liberia zikiwa bado hazijashuhudia visa vyo vyote kwa miezi kadhaa sasa. Hata hivyo wataalamu wanasema ni sharti nchi ziwe waangalifu kwa ongezeko la visa vipya.
Ebola husambaa kwa kumgusa mtu huku Virusi vyake vikipatikana hupatikana kwenye maji ya mwili – damu- matapishi na mate.