Waziri wa usalama na haki wajiuzulu Ubelgiji

 

Waziri wa usalama wa ndani na waziri wa haki nchini Ubelgiji wajiuzulu kufuatia shambulizi la kigaidi mapema wiki hii.

Kulingana na ripoti kutoka wizara hiyo ni kuwa wawili hao Jan Jambon wa wizara ya usalama wa ndani na Koen Geens waziri wa haki wamechukua hatua hiyo kwakua shambuilizi hilo limeonekana kuwa kuzembea kwa kazi zao hivyo basi kutoa fursa sheria na uchunguzi kufuatia.

Mapema wiki hii watu zaidi ya 30 walipoteza maisha katika shambulizi la kigaidi lililohusisha vilipuzi viwili katika uwanja wa ndege jijini Brussels.