37 wakamatwa katika sakata ya chanjo Uchina

Watu Thelathini na saba wametiwa mbaroni nchini Uchina kwa kuhusika katika sakata ya chanjo.
Hii ni baada ya polisi katika mji wa Shandong kutangaza mwezi uliopita kwamba wamemkamata mama na bintie wanaoshukiwa kununua na kuuza chanjo kinyume cha sheria.
Biashara hiyo haramu inasemekana kuanza tangu mwaka 2011,na hivyo kuzua hasira kali kote nchini Uchina.
Sakata hiyo imesababisha msako mkali, huku ukaguzi ukifanywa miongoni mwa watengenezaji wa chanjo, wauzaji wa jumla na wanunuzi wa bidhaa hiyo.