Watu 7 wauawa katika ajali ya ndege Canada

Watu saba wamefariki baada ya ndege moja ya kibinafsi nchini Canada kuanguka katika kisiwa cha mashariki ya pwani ya Quebec.

Taarifa zinaarifu kuwa ndege hiyo ilianguka ilipokuwa ikikaribia uwanja wa ndege wa Madeleine huku kukiwa na upepo mkali pamoja na barafu.

Jean Lapierre,aliyekuwa waziri wa uchukuzi nchini Canada pamoja na watu wa familia yake walikuwa miongoni mwa waathiriwa.