Viongozi wa EU kuwasilisha pendekezo la kukabiliana na mgogoro wa wakimbizi

Viongozi wa Umoja wa Ulaya walioko kwenye mkutano nchini Brussels wameamua kwa pamoja kuwasilisha pendekezo moja kwa Uturuki, katika kukabiliana na mgogoro wa wakimbizi.
Katika mapendekezo ya mpango uliowekwa,wahamiaji wanaoingia Ugiriki kutoka Uturuki watarudishwa huku Uturuki ikipewa msaada wa kifedha na raia wake kuingia barani ulaya bila visa.
Chansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema Uturuki imekubali kuwapokea wakimbizi ambao wanarudishwa kutoka fukwe za Ugiriki na pia kuhakikisha hawapokei wafanya biashara haramu wa binadamu.
Rais wa Ufaransa, Francois Hollande, amesema kunahitajika makubaliano ambayo yataisaidia Ugiriki pamoja na Uturuki.