Kundi la Kikurdi lakiri kutekeleza mauaji Uturuki

Kundi la wanamgambo wa Kikurdi limekiri kutekeleza shambulizi baya zaidi siku ya Jumapili katika mji mkuu wa Ankara.

Katika taarifa iliotumwa mitandaoni,shambulio hilo lililowauwa watu 37 lilikuwa la kulipiza kisasi oparesheni za kijeshi katika eneo la wakurdi la Kusini Mashariki.

Huku hayo yakijiri Ujerumani imefunga ubalozi wake mjini Ankara pamoja na shule moja mjini Instabul siku ya Alhamisi.

Waziri wa maswala ya kigeni wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier amesema kuwa kuna ushahidi kwamba wapiganaji walikuwa wakijitayarisha kushambulia maeneo manne nchini Uturuki.

Watalii 12 wa Ujerumani waliuawa katika shambulio la kujitolea mhanga linalodaiwa kutekelezwa na wapiganji wa IS mjini Istanbul mnamo mwezi Januari.