Ripoti yasema ushindi wa Trump ni hatari kwa dunia

Shirika moja la kimataifa limesema ushindi wa Donald Trump unachukuliwa kuwa miongoni mwa hatari 10 kuu zaidi zinazokabili dunia.

Shirika hilo la Economist Intelligence Unit limeonya kuwa iwapo Trump atashinda urais Marekani, hilo huenda likavuruga uchumi wa dunia na kuongeza hatari za kisiasa na kiusalama dhidi ya Marekani.

Hata hivyo, shirika hilo halimtarajii Trump, anayeongoza kwenye kinyang’anyiro cha kumchagua atakayepeperusha bendera ya chama cha Republican, kumshinda Hillary Clinton ambaye shirika hilo linasema kuwa ana uwezekano mkubwa sana kuwa mgombea wa chama cha Democratic”.