Korea Kusini kufanya majaribio zaidi ya mabomu

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Un ameamrisha majaribio zaidi ya kinyuklia yakutumia mabomu yasiyokuwa na nguvu, ambayo anasema wanasayansi wa nchi yake wametengeneza.
Awali kiongozi huyo alisema wanasayansi wa nchi yake wamefanikiwa kupunguza ukubwa na mabomu ili yaweze kuwekwa kwenye makombora.
Waandishi wa habari wamesema ikiwa hili litathibitishwa, hili litakua tishio kubwa kwa Korea Kusini na nchi nyingine zilizoko kwenye kanda hiyo.