Wizara moja yapiga marufuku kuchati wakati wa kazi Tanzania

social-media-icons-generic-ss-1920-800x450

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania imewapiga marufuku wafanyakazi wake kuchati katika mitandao ya kijamii katika muda wa saa za kazi.

Waziri wa Wizara hiyo Makame Mbarawa amelaani vikali tabia ya baadhi ya wafanyakazi, kutumia muda mwingi  katika mitandao ya kijamii  hali inayosababisha kushuka kwa uzalishaji na maendeleo.

Ameongeza kuwa watakaobainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria na pia kuwataka wafanyakazi wa wizara yake kuwa na bidii ya kazi.