Ajali mbaya yauwa watu na ng’ombe Tanzania

Watu kadhaa na ng`ombe kadhaa wamefariki pamoja katika ajali iliyohusisha lori aina ya canter na matatu aina ya minibus nchini tanzania eneo Tabata Matumbi.
Kulingana na walioshuhudia ajali hiyo ni kuwa lori hiyo ilikuwa imebeba ng’ombe waliokuwa napelekekwa kichinjioni iligongana ana kwa ana na basi hiyo ambayo ilikuwa ikienda kwa kasi na ilikuwa imebeba watu kupita kiasi.
Hatahivyo maafisa wa trafiki wamefika sehemu hiyo huku jamii na maafisa wa huduma ya kwanza wakishirikiana kuondoa miili na majeruhi kusafirishwa kwenye hospitali za karibu.