Al-shabaab yathibitisha kushambuliwa na Marekani

images (3)

Kundi la wanamgambo wa Al-Shabaab nchini Somalia limethibitisha kwamba maeneo yake yalishambuliwa kwa mabomu na Marekani.

Hata hivyo, kundi hilo limesema taarifa kwamba zaidi ya wanamgambo 150 waliuawa kwenye mashambulio hayo yaliyotekelezwa na ndege zisizo na rubani ni za kupotasha.

Wizara ya ulinzi ya Marekani ilisema wapiganaji 150 wa al-Shabab waliuawa kwenye mashambulio yaliyotekelezwa Jumamosi katika kambi ya mazoezi ya wanamgambo hao.

Hata hivyo hakusema ni wapiganaji wangapi wa kundi hilo waliuawa.