Bomu la laptop lalepuka na kujeruhi 6 Somalia

Watu 6 wamejeruhiwa katika mlipuko uliotokea katika uwanja wa ndege ulioko mjini Beledweyne nchini Somalia.
Wawili kati ya waliojeruhiwa ni maafisa wa polisi huku wengine wakiwa raia.
Bomu hilo linaaminika kuwa limetegwa ndani ya kipakatilishi.
Mwezi uliopita,kundi la kiislamu la Al-Shaabab lilidai kutekeleza shambulizi lililosababisha shimo kutokea katika ndege moja ya abiria.
Shambulizi hilo lilitekelezwa na bomu lililotegwa ndani ya kipakatilishi.
Afisa wa ulinzi katika eneo hilo Luteni Kanali Ali Dhuh Abdi amesema kuwa bomu hilo lililipuka kisha maafisa wa usalama wakaharibu mabomu mengine 2 yaliyokuwa yametegwa ndani ya kipiga chapa.