Rubani afariki angani baada ya kupata mshtuko wa moyo

Saudi Arabian 777-300ER Artwork K65053
Rubani mmoja wa ndege amefariki wakati alipokuwa angani baada ya kuugua maradhi ya mshtuko wa moyo katikati ya safari nchini Saudi Arabia usiku wa kuamkia leo.
Hali ya taharuki ilitanda katika ndege hiyo ya shirika la Saudi Arabian Airlines iliyokuwa na abiria 220 wakati rubani Mohammed Al-Mohammed alipofariki ghafla.
Duru zinaarifu kuwa ndege hiyo ilikuwa inaelekea katika uwanja wa ndege wa King Khalid mjini Riyadh kutoka uwanja wa Bisha Kusini Magharibi mwa Saudia,kabla ya tukio hilo kujiri muda mchache kabla ya kutua.
Hata hivyo maafisa wakuu wa shirika hilo la ndege wamempongeza rubani mwenza wa ndege hiyo Rami Ben Ghazi kwa ujasiri wake wa kudhibiti chombo hicho hadi kilipotuwa.