Crown kufungua kampuni mpya Kisumu

Waziri wa viwanda na biashara nchini Adan Mohamed anatarajiwa kufungua kiwanda kipya cha rangi cha Crown katika kaunti ya Kisumu, ambacho kitagharimu shilingi bilioni 3.
Inaarifiwa kiwanda hicho kitazalisha zaidi ya Lita elfu 800 za rangi katika kipindi cha mwezi mmoja, pamoja na kutoa nafasi za ajira kwa zaidi ya watu elfu moja.
Mohamed amesema hatua hiyo ni kati ya miradi ya serikali ya kuona kuwa sekta ya biashara nchini inaimarika.