Malipo ya ardhi na leseni za biashara kulipwa kidigitali

download (7)

Serikali ya kaunti ya Nairobi imesema kuanzia mwaka ujao wa fedha haitakubali malipo ya ardhi na leseni za biashara kupitia pesa taslimu katika kaunti hiyo.

Waziri wa mawasiliano na teknolojia wa kaunti hiyo Anne Lokidor amesema malipo ya kupangisha, kuegesha magari, na idhini ya ujenzi yatafanywa kupitia mfumo wa kidijitali.

Serikali hiyo imesema mfumo huo unalenga kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kurahisisha utowaji wa huduma bora.