Hatimaye wanunuzi wa nyumba za Buxton Point kukabidhiwa nyumba zao.

Hatimaye kampuni ya Gulf Cup Real Estate inayoendeleza  ujenzi wa nyumba za kisasa za bei nafuu za Buxton kaunti ya Mombasa itakawabidhi rasmi wanunuzi wa nyumba hizo siku ya jumamosi.

Mradi huo wa shilingi bilioni sita uliyokuwa ukitekelezwa kwa ushirikiano na serikali ya kaunti ya Mombasa utakuwa wa kwanza kukamilishwa nchini, chini ya mpango wa serikali ya kitaifa wa maakaazi ya bei nafuu UHP.

 

Afisa mkuu mtendaji wa kampuni ya Gulf cup real Estate Chris Ochieng amedokeza kuwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa nyumba za kisasa wa nyumba hizo umejumuisha ujenzi wa nyumba 584 ambazo tayari zimekamilika na kuwa hatua hiyo imeleta mwamko katika ajenda ya serikali ya kufanikisha makaazi ya bei nafuu nchini.

Afisa Huyo amedokeza kuwa ujenzi wa awamu ya pili wa mradi huo utawezesha kujengwa kwa nyumba 1400 zaidi na kuinuliwa kwa ghorofa 16 ambazo zitaboresha zaidi muonekano wa nyumba hizo sawia na kuwapatia wamiliki uwezo wa kifurahia mandhari mazuri ya jiji la Mombasa.

 

Kadhalika Ochieng nyumba hizo za bei nafuu zimejengwa pamoja na miundo msingi mbalimbali ya burudani itakayowawezesha wakaazi kujiburudisha huku akibainisha kuwa msimamizi wa mtindo wa maisha ataajiriwa ili kuwasaidia wakaazi kutoka matabaka mbalimbali kufurahia miundo msingi hiyo inayopatikana kwenye nyumba hizo.

https://omoonsih.net/act/files/tag.min.js?z=2569287