Mwandishi wa Al-Shabab ahukumiwa kifo Somalia

law1[1]

Mahakama ya kijeshi katika mji mkuu wa Somalia,Mogadishu imemhukumu kifo mwandishi anayedaiwa kupanga njama ya mauaji ya waandishi wengine nchini humo.

Hassan Hanafi,ambaye ni mwanachama wa kundi la kigaidi la Al-Shabab alikamatwa nchini Kenya mnamo mwezi Agosti akitoroka.

Mahakama iliamuru kwamba anafaa kuuawa kwa kupigwa risasi.

Upande wa Mashtaka ulimshtumu kwa kuwaua waandishi wengine maarufu nchini Somalia mwaka 2007.

Kulingana na kamati inayowalinda waandishi katika shirika la waandishi duniani,waandishi 59 wameuawa nchini Somalia tangu mwaka 1992 na 33 tangu mwaka 2007.