Rais kufungua waonyesho ya kilimo ya Eldoret mwezi ujao

Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kufungua rasmi maonyesho ya kilimo mjini Eldoret tarehe nne mwezi ujao huku maandalizi ya maonyesho hayo yakiwa yamenoga.
Mwenyekiti wa maonyesho hayo WycLiff Nangalama amesema kauli mbiu ya mwaka huu ni matumizi ya teknologia katika kuimarisha kilimo na viwanda.
Mataifa jirani ya Uganda na Tanzania pia yatashiriki maonyesho hayo yatakayoanza tarehe mbili hadi tarehe tano mwezi ujao.