Wanajeshi 3 wauawa katika shambulizi Mali

gggg
Wanajeshi watatu wameripotiwa kuuawa katika shambulizi nchini Mali.

Wizara ya Ulinzi nchini humo imethibitisha tukio hilo ingawa haikusema sehemu lilipotokea shambulizi hilo.

Serikali ya Mali ambayo hivi sasa iko katika mazingira magumu ya kutekeleza makubaliano ya amani na wapinzani, katika miezi ya hivi karibuni imekumbwa na mashambulio kadhaa ya kigaidi.

Eneo la kaskazini mwa Mali limekuwa likishuhudia machafuko tangu mwaka 2012 wakati makundi yanayotaka kujitenga yalipoteka maeneo kadhaa.