Uchumi wa Afrika Kusini wazorota

pravin-gordon-minister-finance

Waziri wa fedha nchini Afrika Kusini,Pravin Gordhan amesema kuwa uchumi wa nchi hiyo uko katika hali mbaya.

Katika hotuba yake ya bajeti alisema kuwa takwimu za ukuwaji wa uchumi wa taifa hilo zimeshuka kutoka asilimia 1.7 hadi 0.9.

Waziri huyo amesema kuwa uchumi unazorota kutokana na kupungua kwa ukuaji wake,ukosefu wa ajira na kuenea kwa umasikini.

Gordhan,alitarajiwa kutangaza mipango ya kubinafsisha mali ya serikali,lakini alisema kuwa mipango inaendelea ya kuunganisha shirika la ndege la taifa hilo na shirika la ndege linalomilikiwa na serikali la SA Express.