Nkurunziza akubali kufanya mazungumzo na upinzani

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa,Ban Ki-moon amesema kuwa rais Pierre Nkurunziza ameitikia mwito wa mazungumzo ya upatanishi yanayolenga kumaliza miezi 10 ya mzozo wa kisiasa.
Ban ambaye yuko mjini Bujumbura katika ziara maalum amesema kuwa Nkurunziza pia amekubali kuwaachilia huru wafungwa 2000.
Makabiliano yalianza mwezi Aprili mwaka jana rais Nkurunziza alipotangaza azma yake ya kuwania awamu ya 3 ya urais katika uchaguzi mkuu.
Wapinzani wake walidai kuwa rais huyo alikuwa anakiuka katiba ya nchi hiyo inayomtaka kiongozi asitawale kwa zaidi ya vipindi viwili.