Ban Ki Moon awasili Burundi kutatua mzozo wa kisiasa

Ban-Ki-Moon-300x200

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon anatarajiwa kukutana na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza katika juhudi za kutatua mzozo wa kisiasa nchini humo.

Ban,aliyewasili nchini Burundi Jumatatu, atakutana na  Nkurunziza leo katika ikulu na baadaye wawili hao wanatarajiwa kutoa taarifa ya pamoja.

Jana,Ban alikutana na wawakilishi wakuu wa vyama vya siasa na kujadili amani na usalama nchini humo.

Mamia ya watu wameuawa na maelfu kutoroka makwao tangu kuanza kwa machafuko nchini humo mwezi Aprili mwaka jana baada ya Rais Nkurunziza kutangaza azma yake ya kuwania urais kwa muhula wa tatu.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma,pamoja na Rais wa Gabon Ali Bongo na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn
wanatarajiwa kufika Burundi siku ya Alhamisi kufanikisha mazungumzo ya kutafuta amani.