Uchaguzi ulikuwa wa haki asema Museveni

99103-004-087D32E9

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kuwa uchaguzi uliofanyika nchini humo Alhamisi wiki iliyopita ulikuwa wa haki na akasema wanaoutilia shaka hawaielewi Uganda.

 

Upinzani umedai kuwepo kwa wizi wa kura na waangalizi wa kimataifa wamesema pia kwamba hakukuwa na nafasi sawa ya ushindani.

Waangalizi wamelalamikia kukamatwa kwa Dkt Kizza Besigye,kucheleweshwa kwa kufunguliwa kwa vituo vya kupigia kura na kuzimwa kwa mitandao ya kijamii.

Mkuu wa waangalizi wa Jumuiya ya Madola,Olusegun Obasanjo, amesema matatizo mengi katika utaratibu wa uchaguzi yametia shaka uaminifu na uhaki wa shughuli nzima ya upigaji kura nchini humo.