Biashara ya maua kuimarika

Nairobi-flowers

Wafanyibiashara wa maua nchini wanamatumaini ya kuimarika kwa biashara yao wakati ambapo baadhi ya wananchi wanaelekea katika sherehe ya siku ya wapendanao.

Mkurugenzi wa baraza la maua nchini Jane Ngige amesema kuwa wafanyibiashara hao husafirisha takriban asilimia 30 ya mazao yao katika mataifa jirani wakati sherehe hiyo.

Asasi ya takwimu ya kitaifa imesema viwanda vya maua viliingiza shilingi bilioni 54.6 kwa kusafirisha nje bidhaa hiyo mwaka jana, ambayo ni asilimia 27 ya shilingi bilioni 42.8 zilizopatikana mwaka 2012.