“Serikali Yakosa kuwajibikia maendeleo kwa wakenya,” asema Kimani Ngunjiri.
Mbunge wa Bahati katika kaunti ya Nakuru Kimani Ngunjiri kwa mara nyingine ameilaumu serikali kwa kutowafanyia wakenya maendeleo.
Kulingana na Ngunjiri, ajenda kuu nne za serikali ambazo ni Afya kwa Wote, Makazi Bora, Ukuaji wa Viwanda na Utoshelezo wa Chakula na ambazo rais Uhuru Kenyatta aliahidi kwa wakenya, zimelemazwa na baadhi ya viongozi ambao wanapigia debe ripoti ya BBI.
Vile vile Anasema kuwa baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wanalenga kutumia ripoti ya BBI ili kujitafutia uongozi badala ya ripoti hiyo kuwanufaisha wakenya.
Hata hivyo Ameongeza kuwa wakenya ndio watakaoamua ni nani atakayemrithi rais Uhuru Kenyatta katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu ujao mwaka 2022.